Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepongezwa kwa kupata hati safi katika matokeo ya ukaguzi ambao ulifanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwenye hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ulioishia Juni 30, 2023.
Pongezi hizo zimetolewa Julai 13, 2024 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Abbas Mohamed Abbas katika Baraza la madiwani la kujadili taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka wa fedha wa 2022/2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Amesema “Niipongeze Halmasahuri ya Wilaya ya mbinga kwa kupata hati safi ikwa ni matokeo ya ukaguzi amabao ulifanywa na Mdhiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hongereni sana”
Pamoja na pongezi hizo ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuhakikisha unakamilisha mapendekezo ya CAG na kufunga hoja zote zilizobaki ikiwa ni pamoja na maagizo ya LAAC kabla au ifikapo Septemba 30,2024.
Aidha ametoa wito kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kufanya ufuatiliaji wa karibu na kuhakikisha hoja hazizalishwi na kuweka mikakati ya kupunguza hoja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mhe. Desderius Haule amesema kuwa utekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit