MBINGA DC YAPONGEZWA UTEKELEZAJI WA MIRADI
Na Silvia Ernest
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Rwiza kwa kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Halmashauri pamoja na ujenzi wa wodi tatu katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya.
Pongezi hizo zimetolewa tarehe 29 Mei 2024 katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
"Utekelezaji wa miradi unaridhisha nikupongeze Mkurugenzi maboresho madogo madogo ni kama kupanda miti ya matunda miti ya kivuli ili eneo hili livutie" Amesema
Sambamba na pongezi hizo ametoa wito kwa Halmashauri kuhakikisha miundombinu hiyo inatunzwa vizuri na kusisitiza kuwa Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Kwa kipekee Kanali Abbas amempongeza Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bi. Neema Mbilinyi kwa kusimamia utekelezaji miradi, amemtaka kuendeleza ari hiyo ya kutekeleza miradi katika viwango bora.
" Mimi binafsi nina farijika sana nikikuta Mhandisi anaesimamia ujenzi ni mwanamke, umefanya kazi nzuri inaonekana endeleza hiyo ari ya uwajibikaji na uzalendo" Amesisitiza
Ujenzi wa jengo la makao Makuu ya Halmashauri umegharimu shilingi Bil 3.3 hadi kukamilika na ujenzi wa wodi tatu utagharimu shilingi 500,000,000 hadi kukamilika.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inaendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji huo ambao unakwenda kuleta tija kwa wananchi.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit