Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Andrew Mbunda ameishukuru Timu ya Waataalam kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwa kutoa Elimu ya namna bora ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya mnyoo Tegu (Taenia solium) ambao unaathiri afya ya binadamu na nguruwe.
Bw. Andrew Mbunda ameishukuru Timu ya Waataalam kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwa kutoa Elimu ya namna bora ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya mnyoo Tegu (Taenia solium) ambao unaathiri afya ya binadamu na nguruwe.
Bw. Andrew Mbunda amebainisha hayo tarehe 29 Mei 2023 katika kikao kazi cha kuwasilisha matokeo ya tafiti ya mzunguko wa maisha ya mnyoo Tegu uliofanywa na Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika vijiji vya Matiri na Mkumbi vilivyopo katika Halmshauri ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
"Nitoe shukrani zangu kwenu kwanza mmeleta mrejesho wa tafiti maana mngekuwa wengine msingerudi kutoa matokeo lakini pia elimu hii itatusaidia kutoa elimu endelevu kwa jamii" Amesisitiza Mbunda.
Akizungumza katika Kikao kazi hiko Bi. Christina Marwa kutoka Chuo Kikuu cha SUA amebainisha kuwa madhara ya mnyoo huyo kwa binadamu ni pamoja na kusasabisha kupooza mwili, upofu, maumivu ya kichwa ya muda mrefu pamoja na kifafa, hivyo ametoa wito kwa Halmashauri kutoa elimu endelevu kwa jamii ili kujikinga dhidi ya maambukizi hayo.
Kwa upande wake Bw. Innocent Meckriory kutoka chuo cha SUA amebainisha kuwa uelewa wa jamii kuhusiana na madhara yanayosababishwa na mnyoo huyo bado ni mdogo na pia bado kuna maambukizi ya mnyoo huyo kwa binadamu na nguruwe nchini.
Bw. Innocent amesisitiza kuwa elimu endelevu kwa jamii ya namna bora ya kuzingatia usafi wa chakula pamoja na kunywa maji safi na salama ni baadhi ya njia za kudhibiti maambukizi ya mnyoo huyo.
Utafiti huo ulifanyika mwaka 2019 katika Vijiji vya Matiri na Mkumbi vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit