Elimu ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto imeendelea kutolewa kwa jamii katika kipindi hiki cha wiki ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kilele chake kinatarajiwa kuwa Machi 08 mwaka huu 2023.
Elimu hiyo imetolewa kwa wanafunzi wa shule za Sekondari za Mndeme na shule ya sekondari ya Wasichana Mbinga (Mbinga Girls) wakati kamati ya maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Wilaya ya Mbinga ilipotembelea na kuzungumza na wanafunzi wa shule hizo.
Tukio hilo limefanyika Alhamisi tarehe 2 Machi ambapo pamoja na mambo mengine kamati hiyo inayojumuisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi pamoja na asasi za kiraia pia imetoa elimu ya maadili na usawa wa kijinsia kwa wanafunzi hao.
Huu ni mlolongo wa matukio mbalimbali yanayofanyika kwa kipindi chote kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake tangu kufanyika kwa uzinduzi rasmi wa maadhimisho haya Machi Mosi ambapo Mgeni Rasmi alikua Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu 2023 yenye kauli mbiu "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia; Chachu Katika Kuleta Usawa wa Kijinsia" kimkoa yamepangwa kufanyika Mbambabay Wilayani Nyasa ambapo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
imeandikwa na Salum Said
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit