Timu ya uelimishaji jamii juu ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia wilaya ya Mbinga leo Novemba 30 imeshiriki kwa vitendo Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Ukatili Dhidi ya Watoto kwa kutoa elimu kwa umma kupitia Redio Ruvuma FM na Redio Hekima FM.
Pamoja na utoaji wa elimu kwa umma kupitia vipindi vya redio timu hiyo imefanikiwa pia kuwatembelea na kuzungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiwanjani na Shule ya Sekondari Ruhuwiko juu ya athari mbalimbali za vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto na namna watoto hao wanavyoweza kusaidia kupambana na vitendo hivyo kwa kuripoti matukio yanayotokea kwenye ngazi na mamlaka zinazohusika katika maeneo yao.
Timu hiyo iliyoundwa kuratibu kampeni hii ya kupinga vitendo vya ukatili inajumuisha Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri za Wilaya na Mji wa Mbinga, Maafisa wa Dawati la Jinsia Kituo cha Polisi Wilaya ya Mbinga pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo taasisi ya SMAUJATA.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
Tarehe 30 Novemba, 2022
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit