Jumla ya miradi 9 yenye thamani ya shilingi milioni 325.94 imetembelewa katika Kata 4 za Mpapa, Nyoni, Kigonsera na Mkako ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Mwenge wa Uhuru uliopokelewa Kijiji cha Burma, Kata ya Mpapa ukitokea Wilayani Nyasa Jumamosi Tarehe 9 Aprili, 2022
Akiwasilisha taarifa mara baada ya kuhitimishwa kwa Mbio za Mwenge wa Uhuru ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Juma Haji Juma amesema katika mbio za Mwenge mwaka huu miradi mitatu yenye thamani ya shilingi milioni 77.3 imekaguliwa, miradi 5 yenye thamani ya Tshs. Milioni 231.1 ikifunguliwa.
Aidha Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa mradi mmoja wa bajaji wenye thamani ya Tshs. Milioni 17.45 ukishindwa kukabidhiwa kwa Kikundi cha Vijana Fastafasta huku Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma akitoa maelekezo ya bajaji hizo kukatiwa bima kubwa (comprehensive) badala ya bima ndogo (third party).
Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2022 ni Shamba Bora la Kahawa, Shamba la Miti (Kijiji cha Burma), Mradi wa Maji wa mtu binafsi, Ufunguzi wa Zoezi la Tohara na Ugawaji wa Vyandarua zahanati ya kijiji cha Kigonsera (Kijiji cha Kigonsera).
Miradi mingine ni Ufunguzi wa Anwani za Makazi na Postikodi, Klabu ya Lishe, Klabu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB Club) na Ufunguzi wa Vyumba 3 vya Madarasa yaliyojengwa kupitia mradi Na.5441 TCRP (UVIKO-19) Shule ya Sekondari Mkako yote hii ikiwa ikitembelewa katika Kijiji cha Mkako.
Imeandikwa na
Salum Said, Mbinga DC
Tarehe 10 Aprili, 2022
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit