MKOA WA RUVUMA WATOA MAFUNZO YA SIKU MBILI YA UTOAJI WA CHANJO KWA WATAALAMU WA AFYA NA MAAFISA HABARI.
Na VINCENT J. MPOMBO-MBINGA DC.
Mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Jairy Khanga alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawewzesha wataalamu wa afya kwenda kutoa huduma za chanjo kwa wananchi kwa kutoa elimu ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuchanja.
Dkt Khanga amedai mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu wa afya hao watawezeshwa njia na mbinu za kuelimisha jamii pamoja na kupambana na changamoto zitakazopatikana kutoka kwa wananchi aweze kutoa elimu ya kuwaelimisha wananchi na waweze kuchanjwa.
‘’Wananchi hawana taarifa sahihi kuhusu chanjo ndio maana mwamko wa wananchi katika swala la kuchanja ni dogo hivyo tunatakiwa kuimarisha dhana ya mawasiliano na kuwafanya wananchi wengi waweze kupata tarifa sahihi na kubadilisha fikra potofu walizonazo na wakubali kuchanja alisema” Dkt Khanga
Hata hivyo aliwataka watoa huduma za chanjo katika mkoa wa Ruvuma kushiriki mafunzo ya siku mbili ya kujengewa uwezo katika utoaji chanjo katika Halmashauri za wilaya zote za mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuwafanya wananchi wahamasike katika zoezi la kuchanja.
Aidha pamoja na mambo mengine alimpongeza afisa afya mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru bwana Arnold Herman na mratibu wa elimu ya afya kwa jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Ally Yassin Ndambile kwa kuhamasisha jamii kuhusu kupata chanjo.
William Reuben kiongozi wa timu ya kitaifa ya chanjo katika mkoa wa Ruvuma amewataka washiriki wa mafunzo kuleta matokeo katika kazi watakazotakiwa kwenda kuzifanya ili kutekeleza lengo la saerikali la kuhakikisha wananchi wake wanapata chanjo .
Mada zinazofundishwa katika mafunzo hayo ni mada 8 ambapo kwa siku ya kwanza mada ya sayansi ya jamii,mawasiliano juu ya chanjo ,mabadiliko ya tabia , utaratibu na usimamizi shirikishi kwa jamii na mada zingine 4 zitafundishwa siku ya pili.
Mwisho.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit