Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Juma Haji Juma amezitaka kamati za ujenzi zinazohusika katika ujenzi wa matundu ya vyoo 17 katika Shule ya Msingi Nimbua kuimarisha usimamizi wakati wa mapokezi na matumizi ya vifaa vinavyotumika katika ujenzi huo.
Amebainisha kuwa kutokuwa makini wakati wa mapokezi na matumizi ya vifaa vya ujenzi kunapelekea upotevu wa vifaa na taarifa zisizo sahihi.
Mkurugenzi ametoa rai hiyo katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa matundu ya vyoo 17 yanayojengwa katika Shule ya Msingi Nimbua iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
"Kamati zote zinazohusika na utekelezaji wa ujenzi huu hakikisheni mnaimarisha usimamizi hii itasaidia kuwa na taarifa sahihi ya mapokezi na matumizi ya vifaa" Amebainisha
Ujenzi wa matundu ya vyoo 17 katika shule ya Msingi Nimbua Unatekelezwa kupitia Mradi wa SWASH na unagharimu Shilingi Mil. 41,116,795.42
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit