Na Silvia Ernest
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura 22 Agosti 2024 ametembelea na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya unaoendelea kutekelezwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Huu ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Lengo likiwa ni kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakamilika kwa wakati, katika ubora ili kuondokana na miradi viporo.
Ametembelea jengo la mionzi, jengo la wazazi ( Martenity Complex) ambalo limekamilika na huduma za kujifungua kwa njia ya kawaida zinatarajia kuanza tarehe jumatatu tarehe 26 Agosti 2024 pamoja na ujenzi wa wodi tatu ( Wanawake, wanaume na watoto) ambazo utekelezaji wake bado unaendelea.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit