Mkuu wa wilaya ya Mbinga Mh.COSMAS NSHENYE (wakwanza kulia) leo ameongoza zoezi la kugawa pikipiki kwa Maafisa elimu kata wa Mbinga . Zoezi hilo limefanyika katika ofisi za mkurugenzi mtendaji leo majira ya saa 9:30 jioni.
Kabla ya zoezi hilo kuanza Mh. Samweli Komba mbaye ni afisa elimu msingi wilaya ya Mbinga alisoma taarifa fupi mbele ya uongozi wa wilaya na umati uliokusanyika eneo hilo kushuhudia zoezi hilo la ugawaji wa pikipiki.
Mh.Samweli Komba alisema serikali imetoa pikipiki hizo ili kuwasaidia maafisa elimu hao katika shughuli zao za kikazi.Pia alisisitiza kuwa pikipiki hizo zitumike kwa shughuli za kikazi tu na zisaidie kutokomeza tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma kuandika na kuhesabu.
Mh. Samweli Komba aliwasihi maafisa elimu kata hao wasizitumie pikipiki hizo kwa maswala ya biashara mfano bodaboda, kubebea mazao, na kukodisha. Alisema atakayebainika atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Aidha Mh. COSMAS NSHENYE ambaye ni Mkuu wa wilaya ya mbinga aliwasihi pia maafisa elimu hao kuwa wasije chezea vyombo vya serikali kwa maslahi yao binafsi. Aliwaeleza maafisa hao wahakikishe kabla ya kuanza kuzitumia wawe na leseni.Alisema pikipiki hizo zikatumiwe kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo. Kisha alifungua zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa kuzindua kuendesha pikipiki moja.,
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit