Mkuu wa wilaya ya Mbinga Ndg. Cosmas Nshenye amefungua rasmi msimu mpya wa uuzaji wa zao la Kahawa Wilayani Mbinga tarehe 29/06/2018. Katika ufunguzi huo Mhe. Mkuu wa wilaya alieleza kuwa msimu huu umetoa fursa kwa Wakulima kuuza zao la Kahawa kupitia vyama vyao vya Msingi (AMCOS).
Akihutubia wadau mbalimbali wa kahawa na viongozi wa vyama vya msingi Mhe. Mkuu wa wilaya ya Mbinga alisema kuwa uuzwaji wa zao la kahawa kupitia Ushirika kwa msimu huu ni kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) kwamba Wakulima wote wa zao la kahawa lazima waunde vikundi (AMCOS) na kahawa yao itatoka kwenye hizo AMCOS kwenda kuuzwa mnadani kupitia chama kikuu cha Ushirika, hii ni kutekelezwa kwa ilani ya chama 2015 chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Mkuu wa wilaya aliwaasa wakulima wa kahawa kuwa ni lazima kahawa ikusanywe na kutunzwa vizuri kwa kiwango chenye ubora ili kuweza kujipatia soko nzuri litakaloweza inua pato lao na Taifa kwa ujumla ili kufikia maisha bora ambapo mkulima anaweza kujipatia stahiki (mahitaji) mbalimbali bila wasiwasi.
Aidha Mheshimiwa mkuu wa Wilaya alisisitiza usimamizi na kudhibiti utoroshaji pamoja biashara isiyo rasmi (Magoma) kwa zao la kahawa ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa vyama vya Msingi kupitia wataalamu husika wa kilimo ili kuona utekelezaji wa agizo la Wazili Mkuu linafikiwa.
Kwa namna ya pekee, Viongozi wa vyama vya Msingi walipendekeza Taasisi za Kifedha kuwapatia Fedha kwa wakati ili waweze kukidhi mahitaji yao kijamii ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa pembejeo kwa lengo la kuboresha mazao yao shambani.
Kutokana na sensa iliyofanyika baada ya agizo la Waziri Mkuu, Wilaya ya Mbinga ina jumla ya wakulima wa zo la kahawa takribani 12,146 ambao wanajumla ya Hekta 7973.24 na wana jumla ya AMCOS- 14 kwa Mbinga Mji na chama Kikuu kimoja cha Ushirika MBIFACU. Makisio ya uzalishaji wa kahawa kwa msimu 2018/19 ni zaidi ya Tani 3,000.
Akifunga kikao hicho cha ufunguzi wa msimu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Ndg. Ndunguru Kipwele aliwataka viongozi hao kuimarisha Ushirika ili kuwa na nguvu kama miaka ya zamani ili kuachana na ubadhilifu uliosababisha Chama Cha Ushirika MBICU kufilisika. Hivyo kuwa na Ushirika wenye nguvu utakuwa ni Mkombozi kwa Mkulima wa Mbinga.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit