MWENGE WA UHURU KUKIMBIZWA KM 1,289.50 MKOA WA RUVUMA
Na Silvia Ernest, Tunduru
Mkoa wa Ruvuma unatarajia kukimbiza Mwenge wa Uhuru umbali wa Kilomita 1,289.50.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas tarehe 8 Juni 2024 katika mapokezi ya mwenge wa Uhuru yaliyofanyika katika Kijiji cha Sauti Moja Wilaya ya Tunduru.
" Katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mwenge wa Uhuru utakimbizwa KM 284, Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo KM 170, Halmashauri ya Wilaya ya Songea KM 134.8, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga KM 110.30,
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa KM 186.6, Halmashauri ya Mji Mbinga KM 140.5, Halmashauri ya Manispaa ya Songea KM 98.20 na Halmashauri ya Wilaya ya Madaba KM 165.10" Amebainisha Kanali Abbas
Kanali Abbas ameongeza kuwa jumla ya miradi 72 yenye thamani ya shilingi 46,101,114,953.76 iliyopo ndani ya Mkoa wa Ruvuma itafikiwa na Mwenge wa Uhuru.
" Miradi 17 itafunguliwa yenye thamani ya 5,714,686,491.95, miradi 13 itawekwa jiwe la Msingi yenye thamani ya 10,604,369,677.69 na miradi 42 itatembelewa yenye thamani ya shilingi 29,782,085,784.12" Amebainisha
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit