Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga Ndg. Pendo Ndumbaro amewataka washiriki wa Mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa matumizi ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuwa mabalozi wa mpango huo katika maeneo yao ili kuhamasisha ushiriki wa wananchi wakati wa utekelezaji.
Ndumbaro ametoa wito huo 18 Julai 2023 katika Mkutano wa Wadau wa kujadili mpango wa matumizi ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga uliofanyika katika Shule ya Sekondari Kigonsera.
" Mradi huu umekuja katika Halmashauri yetu ni wa kwetu utekelezaji wa mradi huu unatuhitaji sisi wananchi nitoe wito kwenu washiriki wa mkutano huu mkawe mabalozi katika maeneo yenu" Amesisitiza Ndumbaro
Amesisitiza kuwa lengo la mradi huu ni kuwezesha umilikishwaji wa ardhi kwa wananchi pamoja na kudhibiti kuongezeka kwa migogoro miongoni mwa watumiaji wa ardhi hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kufanikisha utekelezaji.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbinga Ndg. Andrew Mbunda ameishukuru Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambao unatekelezwa kupitia Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za ardhi ( LTIP).
Amehaidi kusimamia utekelezaji huo kikamilifu ili kuwanufaisha wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit