OCD wa Halmashauri ya Mbinga Ramia Mganga(katikati pichani), amewataka waratibu elimu kata za Halmashauri ya Mbinga Vijijini kutumia pikipiki walizogawiwa kwa
umakini ili zisije zikawatoa uhai au kuwapa ulemavu. Hayo alieleza wakati wa ugawaji wa pikipiki kwa Waratibu wa Elimu wa Kata 29 tarehe 30/ July /2018.
Aidha amewataka waratibu hao kutunza kwa umakini pikipiki hizo ili zisije zikaibiwa " Nawasihi kuweni makini na utunzaji wa pikipiki hizo kwani zikipote
na wewe ndio ulie kabidhiwa na sisi kama Jeshi la Polisi tutaanza uchunguzi na wewe", pia ameagiza kuwa siku ya jumamosi ambayo ni tarehe ni tarehe 4/August /2018
saa nne asubuhi kuhudhulia mafunzo ya sheria barabarani ili kuwajengea uwezo na uelewa zaidi wa sheria na matumizi sahihi ya vyomboi vya moto.
Waratibu elimu kata waliahidi kuhudhulia mafunzo hayo yasiku ya jumamosi na kutii sheria za barabarani
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit