Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amebainisha kuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewekeza zaidi ya Bilioni 4 katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Dkt. Mollel amebainisha hayo 22 Oktoba 2023 alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango katika Uzinduzi wa Chuo cha Afya Litembo kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Aidha katika kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi Mhe. Rais amekuwa kiunganishi kikubwa katika kuhakikisha sekta binafsi zinatimiza azma ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi wote wa Tanzania.
“Leo nipo hapa Litembo katika uzinduzi wa Chuo cha Afya Litembo hii ni sehemu moja wapo ya Serikali kuendelea kuimarisha mashirikiano na Sekta binafsi nchini ili kuleta maendeleo kwa Taifa”, ameeleza Dkt. Mollel
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Aziza Mangosongo amesema chuo cha afya Litembo kitakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma na jirani kwani watazalisha wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya watakaohudumu katika vituo vya kutolea Huduma za afya nchini.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit