Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Balozi Brig. Jen. Wilbert Ibuge leo Juni 12 ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
R.C Ibuge ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo unaojengwa na SUMA JKT, eneo la Kiamili ambapo amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji, Juma Mnwele kwa usimamizi na utekelezaji wa mradi huo.
Mkuu huyo wa Mkoa pia amepongeza jitihada zinazofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga katika kuwezesha jamii kupitia vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ikiwemo kikundi cha vijana cha Chipukizi ambacho kinajishughulisha na ufyatuaji wa tofali zinazotumika kwenye ujenzi wa jengo hilo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Kikundi cha Chipukizi kilichopo Kata ya Kigonsera mwaka huu 2021 kimenufaika kwa kupatiwa mkopo wa shilingi Milioni 22, ni miongoni kwa vikundi vingine zaidi ya 20 ambavyo vimewezeshwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 330 ikiwa ni asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa mwaka wa fedha 2020/21 na 2021/2022.
Imeandikwa na
Salum Said
Afisa Habari, Mbinga DC
12 Juni, 2021
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit