Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amezindua madarasa mawili ya awali yaliyojengwa shule ya Msingi Kipapa iliyopo tarafa ya Hagati Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Tukio hilo limefanyika leo tarehe tarehe 27 Aprili 2023 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni muendelezo wa shughuli zinazofanyika kwenye maeneo mbalimbali Wilayani Mbinga katika wiki hii ya maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akiwasisilisha taariya mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kipapa Saulo Komba amesema mradi huo unaojumuisha ujenzi wa madarasa mawili, matundu 6 ya vyoo, meza na viti pamoja na mfumo wa maji hadi kukamilika kwake umegharimu shilingi Milioni 57.9 ambapo utekelezaji wake ulianza Agosti 2022 na kukamilika Novemba 2022.
Mara baada ya uzinduzi wa mradi huo RC Thomas amepongeza juhudi zilizofanywa na uongozi wa shule, Halamashauri ya kijiji cha Mpapa na Wilaya katika kusimamia kikamilifu mradi huo na kutoa wito kwa wanafunzi, walimu na jamii nzima kuzingatia ulinzi na utunzaji wa miundombinu ya shule hiyo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amekemea wimbi la matukio yanayosababishwa na mmomonyoko wa maadili na kusisitiza kuwa suala la malezi ya watoto linapaswa kuwa jukumu la jamii nzima katika kulea na kufatilia maadili ya watoto.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amechangia mifuko 10 ya saruji katika kuunga mkono jitihada za wananchi wa kijiji cha Kipapa kwa kuanzisha ujenzi wa darasa kwa nguvu zao ambalo bado lipo hatua ya awali ya ujenzi wake huku pia akishiriki zoezi la upandaji wa miti kwenye shule hiyo ambapo miti 400 imepandwa.
Imeandikwa na Salum Said,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
27 Aprili 2023.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit