Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Mkoani Ruvuma zimeanza rasmi leo Jumatatu tarehe 17 Aprili 2023 mara baada ya kuhitimisha ratiba yake Mkoani Lindi na zitahitimishwa Aprili 25 kwa kuukabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Njombe
Sherehe za makabidhiano ya Mwenge huo zimefanyika Wilayani Tunduru katika kijiji cha Sautimoja mapema majira ya saa 3 asubuhi ambapo Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Stephen Ndaki ameupokea Mwenge pamoja na timu ya wakimbiza Mwenge kitaifa kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Bi.Zuwena Omar Jiri.
Mara baada ya tukio la mapokezi kutoka Mkoa wa Lindi naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma ameweza kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro kuashiria kuanza rasmi kwa mbio za Mwenge Mkoani Ruvuma kwa mwaka huu 2023.
Ukiwa Mkoani Ruvuma Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwenye Halmashauri nane zilizopo ndani ya Wilaya tano ambazo ni Tunduru, Wilaya ya Namtumbo, Songea, Mbinga na Wilaya ya Nyasa.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inatarajia kupokea Mwenge huo sikumya Jumamosi tarehe 22 Aprili ambapo baada ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi kwenye maeneo mbalimbali utalala Matiri kabla ya Jumapili kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Mji Mbinga.
Mbio za Mwenge Mkoa wa Ruvuma zinatarajiwa kutamatika Aprili 24 kwa kukimbizwa Wilaya ya Nyasa kabla ya kukabidhiwa Mkoa wa Njombe kupitia Wilaya ya Ludewa.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit