Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ametangaza nafasi za ajira 21,200 kwa kada ya Walimu na Afya.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Aprili 12, 2023 Jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amesema idadi ya watakaoajiriwa katika kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za msingi na Sekondari na kada ya afya 8,070 watakaofanya kazi katika Hospitali za Wilaya, Vituo vya afya na Zahanati
Waziri Kairuki amesema mchakato wa kuajiri watumishi hao umeanza leo Aprili 12 ,2023 hadi hAprili 25, 2023 ambapo waombaji wa nafasi za ajira katika hkada ya ualimu na afya wanatakiwa kuwa wamehitimu kwenye vyuo vya elimu ya juu na kati kwenye fani ya ualimu na afya vinavyotambuliwa na Serikali.
Ameendelea kufafanua kuwa nafasi zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), stashahada (Diploma) na shahada (Degree) ambapo sifa za kitaaluma zimeanishwa kwa waombaji wa kada za ualimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na fani mbalimbali za kada ya afya kama zilivyoainishwa katika tangazo la ajira na katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI
Amesema waombaji wa kada ya ualimu wawe wamehitimu kuanzia mwaka 2015 hadi 2022 na kwa kada ya afya wasizidi umri wa miaka 45, hivyo amewataka waombaji hao kuanza kutuma maombi yao kuanzia leo tarehe 12 Aprili, 2023 hadi 25 Aprili, 2023 saa 5:59 usiku.
Waziri Kairuki amewataka waombaji waliowahi kutuma maombi ya ajira kupitia mfumo wa maombi ya ajira kuhuisha taarifa zao kwenye mfumo wa ajira kupitia kiunganishi ajira.tamisemi.go.tz kwa kutumia namba ya mtihani wa kidato cha nne na nywila au kuomba upya .
Amewataka waombaji wa ajira hizo kuwa tayari kufanyakazi kwenye Halmashauri na vituo watakavyopangiwa, kufanyakazi na mashirika au taasisi zilizoingia ubia na Serikali na baada ya kupangiwa kituo cha kazi hakutakuwa na nafasi ya kubadilishiwa kituo cha kazi
Aidha ametoa rai kwa waombaji wa ajira hizo kupeuka matapeli watakaowapigia simu na kuwataka kutoa fedha kwa ajili ya kupata ajira kwa kuwa ajira hizo ni bure, vigezo na masharti vitatumika katika kuwaajiri watumishi hao
“Natoa rai kwa waombaji, mtu asije akapigiwa simu kuombwa fedha kwa ajili ya kupata ajira hizo, msiingie katika huo mtego kwa kuwa ikibainika hilo limejitikeza toeni taarifa kwa Mamlaka ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya matapeli” amesisitiza Waziri Kairuki.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit