Timu ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga (PLUM Team) leo tarehe 2 Machi imeanza kupatiwa mafunzo ya namna itakavyoweza kutimiza majukumu yake wakati wa utekelezaji wa mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (Land Tenure Improvement Program-LTIP).
Mafunzo hayo ya siku mbili yanayokusudia kuijengea uwezo timu ya utekelezaji wa mradi yanatolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na yanafanyika Kiamili huku yakishirikisha wataalamu kutoka idara na sekta mbalimbali zinazohusika moja kwa moja wakati wa utekelezaji wa mradi ikiwa ni pamoja na sekta za Ardhi, Maendeleo ya Jamii, Mazingira, Kilimo na Mifugo.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit