• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima
  • MIFUMO

TIMU YA WATAALAMU WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA YATEMBELEA MADABA

Tarehe ya kuwekwa: April 6th, 2021

Imeandikwa na:

Salum Said

Afisa Habari

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA.  Aprili 6, 2021

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Juma Mnwele ameongoza Timu ya Wataalamu wa Halmashauri hiyo na kufanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kujionea namna miradi mbalimbali ya maendeleo inavyotekelezwa na Halmashauri hiyo.

Ziara hiyo ya Wataalamu kutoka Mbinga imefanyika leo Aprili 6, 2021 ambapo wamepata nafasi ya kutembelea miradi mikubwa mitatu ya Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W), Nyumba ya Mkurugenzi na Nyumba 6 za Wakuu wa Idara, miradi ambayo imetekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Madaba kwa mafanikio makubwa.

Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya Wataalamu wa Halmashauri zote mbili za Mbinga na Madaba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Juma Mnwele amesema wanatambua na kuthamini namna Madaba wanavyotekeleza na kusimamia miradi yao hususani jinsi walivyokamilisha ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa na wao (Mbinga) wameona ni sehemu nzuri ya kujifunza kupitia wao.

Naye mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Bw. Shafi Mpenda amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na timu yake ya wataalamu kwa kutembelea Madaba na kuongeza kuwa wamefarikija sana na ujio wa timu hiyo na anaamini baada ya ziara hiyo Mbinga itafanya vizuri zaidi ya walivyofanya wao Madaba katika utekelezaji wa miradi yake ya ujenzi mathalani ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W).

Ziara hii ya Timu ya Wataalamu wa Halamshauri ya Wilaya ya Mbinga ni kufuatia Halmashauri hiyo kupokea fedha kiasi cha Tshs. Bilioni Moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, mradi utakaotekelezwa kwa kutumia Force Account, utaratibu unaohusisha Halmashauri kuwa na majukumu na wajibu wa kufanya ununuzi wa vifaa na usimamizi wa ujenzi kupitia kamati mbalimbali badala ya kutumia wakandarasi kama ambavyo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imekamilisha ujenzi wa jengo lake kwa mafanikio makubwa.

 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inatarajia kuanza ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji hivi karibuni katika eneo la Kiamili lililopo ndani ya Mji mdogo wa Kigonsera kwa kutumia Force Account, ujenzi ambao utahusisha usimamizi wa karibu wa wataalamu hao kupitia Kamati za Ujenzi, Ununuzi, Ukaguzi na Mapokezi ambapo kupitia ziara hiyo ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, timu hiyo imepata chachu, morali na ari mpya ya kufanya vizuri ili kuleta ufanisi katika usimamizi wa miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri hiyo

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI September 17, 2024
  • TANGAZO LA HESABU MBINGA DC July 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA MKATABA NAFASI YA MKUSANYA USHURU January 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA- DEREVA NAFASI 2 January 25, 2024
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI KASHUSHURA ATOA MSISITIZO MATUMIZI YA NISHATI SAFI SHULENI

    February 15, 2025
  • MAAFISA TUME WATEMBELEA MBINGA DC

    January 08, 2025
  • WAANDISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA ANGALIZO

    January 09, 2025
  • KASHUSHURA AWAPONGEZA WANANCHI UJENZI WA SHULE

    September 10, 2024
  • Tazama zote/kote

Video

UGAWAJI WA MKAA MBADALA
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit