• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima
  • MIFUMO

"TUMIENI MITANDAO YA KIJAMII KUHABARISHA UMMA" Asema Gerson Msigwa. Aipongeza Mbinga DC kujiendesha kidijitali.

Tarehe ya kuwekwa: February 21st, 2023

Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametoa wito kwa taasisi za Umma nchini kutumia mitandao ya kijamii kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali kupitia taasisi hizo.

Akiwasilisha mada juu ya Mkakati wa Mawasiliano kwa Umma Jumatatu Februari 20, 2023 mbele ya washiriki wa Mkutano wa 107 wa Mwaka wa Wadau wa Elimu kwa Umma unaoendelea mjini Morogoro Bw. Msigwa amesema matumizi ya mitandao ya kijamii imekua ni kiungo muhimu katika kuhakikisha uwepo wa mawasiliano ya uhakika baina ya taasisi na wadau wake na wananchi kwa ujumla.

Amebainisha kwamba kutokana na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia yaliyopo duniani kote, serikali na taasisi zake haina budi kujiendesha kidijitali katika nyanja nzima ya mawasiliano na kuhabarisha umma ili kuendana na kasi ya mabadiliko hayo na hatimaye kuwafikia wadau wengi zaidi.

Ameongeza kuwa bado taasisi nyingi zinategemea radio, magazeti na runinga kama njia kuu za kufikisha habari na taarifa kwa jamii huku kukiwa na wimbi kubwa la wananchi wanaotegemea mitandao ya kijamii kupata habari mbalimbali hivyo amewataka Maafisa Habari na Mawasiliano wa taasisi zote za Umma kuhakikisha wanafungua akaunti kwenye mitandao hiyo ya kijamii na kuhakikisha wanaitumia kikamilifu ili kuwafikia wadau na wananchi wengi zaidi.

"Unakuta taasisi haina hata akaunti moja kwenye mitandao wa kijamii au kama wanazo basi idadi ya wafuasi haizidi 200, nichukue nafasi hii kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kuwa na wafuasi (followers) zaidi ya 2,000 kwenye akauti yao ya Instagram" Amesema Msemaji huyo Mkuu wa Serikali akiitolea mfano Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inavyotumia mitandao ya kijamii katika kuwafikia wadau wake na jamii kwa ujumla.

Aidha, katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa Idara ya Habari MAELEZO amesisitiza kuendelea kuhuishwa kwa tovuti zote za taasisi za Umma na kwamba kwa sasa serikali pamoja na njia nyingine inatumia tovuti hizo katika kupima utendaji kazi wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini.

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limekua likiandaa mikutano hii ya wadau wa elimu kwa umma kila mwaka na kukutanisha Maafisa Habari, Mawasiliano na Maafisa Uhusiano kutoka taasisi mbalimbali za umma pamoja na wadau wengine wa habari ambapo mkutano wa mwaka huu 2023 ni wa 107 ukifuatia baada ya ule wa 106 uliofanyika Iringa mwezi Juni 2022. 


Imeandikwa na Salum Said 

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga 

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI September 17, 2024
  • TANGAZO LA HESABU MBINGA DC July 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA MKATABA NAFASI YA MKUSANYA USHURU January 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA- DEREVA NAFASI 2 January 25, 2024
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI KASHUSHURA ATOA MSISITIZO MATUMIZI YA NISHATI SAFI SHULENI

    February 15, 2025
  • MAAFISA TUME WATEMBELEA MBINGA DC

    January 08, 2025
  • WAANDISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA ANGALIZO

    January 09, 2025
  • KASHUSHURA AWAPONGEZA WANANCHI UJENZI WA SHULE

    September 10, 2024
  • Tazama zote/kote

Video

UGAWAJI WA MKAA MBADALA
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit