• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima
  • MIFUMO

UPASUAJI WA KWANZA WAFANYIKA KITUO CHA AFYA MAPERA

Tarehe ya kuwekwa: July 1st, 2021

Kituo cha Afya Mapera kilichopo Kata ya Mapera, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kimeanza rasmi kutoa huduma ya upasuaji ikiwa ni mara ya kwanza kwa kituo hicho kutoa huduma hiyo.

Huduma hiyo imeanza kutolewa leo Julai Mosi 2021 ambapo jumla ya akina mama wajawazito watatu wamefanyiwa upasuaji na kufanikiwa kujifungua salama, wawili kati yao wakijifungua watoto wa kike na mmoja akijifungua mtoto wa kiume.

Akizungumzia kuhusu upasuaji huo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Dkt. Louis Chomboko, ambaye pia ameongoza zoezi hilo amesema upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa na kwamba akinamama wote watatu waliopata huduma hiyo, na watoto waliozaliwa hali zao zinaendelea vizuri.

"Zoezi la leo ni mwanzo tu, ndio tumeanza kutoa huduma hii ambayo itakua endelevu na ambayo itasaidia wananchi wa maeneo haya na maeneo ya jirani kutolazimika kwenda mbali kwa ajili ya kufuata huduma ya upasuaji kwani kwa sasa huduma hiyo inatolewa hapa Mapera". Amesema Dkt. Chomboko.

Aidha, ameongeza kuwa mkakati na mpango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ni kuendelea kuboresha na kupanua zaidi huduma za afya katika kituo hicho ikiwemo huduma za  Meno na Radiolojia (X-Ray na Ultrasound) ambazo zitaanza kutolewa hivi karibuni.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2019 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ilipokea fedha shilingi milioni 400 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa majengo yanayopewa kipaumbelele ili kuimarisha huduma ya Afya ya Msingi na utoaji wa huduma za rufaa kwenye Kituo cha Afya Mapera, ujenzi ambao ulianza Agosti 2019 na kukamilika Februari 2020.

Miundombinu iliyokamilika kutokana na matumizi ya fedha hizo ni pamoja na Jengo la Upasuaji (Theatre), Jengo la Maabara (Laboratory), Nyumba ya mtumishi inayojitegemea (staff house), Jengo la kufulia nguo (Laundry) na Jengo la Wazazi (Martenity).

Miundombinu mingine ni jengo la kuhifadhia maiti (Mortuary), Kichomeo Taka (Incinerator), Shimo la Kutupia Kondo la nyuma (placenta pit) na Mfumo wa kuvunia maji ya mvua ambayo kukamilika kwa ujenzi huu kumesaidia kuhudumia wakazi zaidi ya 64,000 waliopo Tarafa ya Hagati na meneo mengine ya jirani.

Imeandikwa na
Salum Said,
Afisa Habari, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
Julai Mosi, 2021

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI September 17, 2024
  • TANGAZO LA HESABU MBINGA DC July 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA MKATABA NAFASI YA MKUSANYA USHURU January 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA- DEREVA NAFASI 2 January 25, 2024
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI KASHUSHURA ATOA MSISITIZO MATUMIZI YA NISHATI SAFI SHULENI

    February 15, 2025
  • MAAFISA TUME WATEMBELEA MBINGA DC

    January 08, 2025
  • WAANDISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA ANGALIZO

    January 09, 2025
  • KASHUSHURA AWAPONGEZA WANANCHI UJENZI WA SHULE

    September 10, 2024
  • Tazama zote/kote

Video

UGAWAJI WA MKAA MBADALA
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit