Na Silvia Ernest
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas amethibitisha kuwa uwanja wa maonesho ya Nane Nane Amani Makoro uliopo Kata ya Amani Makoro Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga unafaa kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za nane nane Mkoa wa Ruvuma kwa mwaka 2024.
Ameahidi kwenda kulifanyia kazi ombi la Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Makori la kuomba maadhimisho hayo Kimkoa yafanyike katika uwanja huo.
Hayo yamebainishwa tarehe 30 Mei 2024 katika ziara ya Mkuu wa Mkoa kutembelea na kukagua miundombinu ya uwanja huo.
Aidha ameagiza miundombinu ya viwanja hivyo iendelee kuboreshwa ili kama itaamriwa maadhimisho hayo yafanyike katika viwanja hivyo, tayari mazingira yawe rafiki.
"Viwanja hivi vinafaa nimengalia mazingira yapo rafiki na nimesikia ombi la Mkuu wa Wilaya la kuomba mwaka huu Kimkoa maadhimisho yafanyike katika eneo hili sasa nipeni muda nikafanye maamuzi kati ya hapa na viwanja vya Sinai" Amesisitiza
Akisoma taarifa Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhandisi Evance Haule amesema Uwanja huo ambao upo Kilomita 8 kutoka barabara kuu ya Mbinga- Songea una ukubwa wa ekari 18.8 ulitolewa na wananchi wa Kijiji cha Amani Makoro kupitia Serikali ya Kijiji kwa ajili ya maonesho hayo.
Haule ameeleza kuwa mpangilio wa matumizi ya viwanja katika eneo hilo unahusisha viwanja vya mabanda ya maonesho ya kilimo na mifugo, Wajasiriamali, Huduma za kijamii,Taasisi za Serikali na binafsi, Bustani, Maegesho ya magari, Uwanja wa mikutano, Eneo la burudani pamoja na matumizi mengineyo.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit