Mkuu wa Wiaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo amekabidhi bajaji mbili zenye thamani ya shilingi milioni 17 kwa vijana watano wa kikundi cha FastaFasta ikiwa ni sehemu utekelezaji wa sera ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 za mapato ya ndani kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu unaofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ndani ya mwaka huu wa fedha 2021/2022
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jumatatu Aprili 25, 2022 kwenye Ofisi za Halmashauri zilizopo Kiamili ambapo Mkuu wa Wilaya amezindua na kukabidhi bajaji hizo kwa vijana tukio lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Desderius Haule, Paschal Zacharia ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo, Madiwani ambao ni wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango na watumishi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Bajaji hizo zinatarajiwa kurahisisha huduma ya usafishaji wa abiria kwa wakazi wa Kata za Kigonsera, Mkako na maeneo jirani hususani kati ya Hospitali ya Wilaya, stendi ya mabasi na Ofisi za Halmashauri zinazojengwa ndani ya eneo hilo la Kiamili.
Salum Said, Afisa Habari Mbinga DC
Tarehe 25 Aprili, 2022
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit