Na Silvia Ernest
Vijiji vya Mahilo, Mzuzu pamoja na Kitura ni miongoni mwa Vijiji 103 vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambavyo vinakwenda kunufaika na mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za ardhi ( LTIP) unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Vijiji hivyo vipo katika awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi wa LTIP ambapo katika awamu ya kwanza Vijiji vya Mkalanga, Ndembo, Silo, Mapipili, Linda, Liyombo, Ulolela pamoja na Lukiti vilifikiwa na mpango huo.
Akizungumza katika mkutano na wananchi wa Kijiji cha Mahilo leo tarehe 7 Septemba 2023 Afisa Mipangomiji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Frank Kaseke amesema kuwa umuhimu wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ni pamoja na kuongeza uelewa wa usalama wa ardhi kwa kuzingatia jinsia na makundi maalum, kuwezesha umikilishwaji wa ardhi pamoja na kudhibiti kuongezeka kwa idadi ya migogoro miongoni mwa watumiaji wa ardhi.
Ili kufanikisha utekelezaji wa mpango huo Kaseke ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu wakati wa utekelezaji wa mpango.
"Huu mpango ni shirikishi ndio maana wananchi wote tutashiriki kuanzia mwanzo hadi mwisho wa utekelezaji hivyo nitoe wito kwa wananchi tushirikiane ili tufanikishe malengo ya Serikali yetu" Amebainisha Kaseke.
Kupitia mkutano huo ambao ulifanyika pia katika Vijiji vya Kitura na Mzuzu wananchi walipata elimu ya kutosha juu ya mradi wa LTIP na Mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji, kisha walichagua wajumbe 7 wa Baraza la usuluhishi wa migogoro la kila Kijiji pamoja na wajumbe 8 wa Kamati ya usimamizi ya matumizi bora ya ardhi kwa kila Kijiji.
Hadi kufikia Mei 2027, Mradi wa LTIP umelenga kuvifikia Vijiji 103 kati ya vijiji 117 vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Vijiji vilivyobaki vimepandishwa hadhi kuwa Miji midogo na zoezi hili kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga halihusu Miji midog
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit