Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mbinga ambao Vijiji vyao bado havijafikiwa na umeme kuwa Vijiji hivyo vitapata umeme kabla ya Desemba 30, 2023.
Kapinga amebainisha hayo Oktoba 8, 2023 katika hafla ya uwashaji umeme kupitia Mradi wa REA awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili katika Kijiji cha Litumbandyosi, kilichopo Kata ya Litumbandyosi, Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Amesema “Mhe. Rais ametoa fedha mpate umeme, Niwahikikishie ndugu zangu wa umeme unakuja, tutamsimamia Mkandarasi kuhakikisha nguzo zinakuja na umeme unawaka"
Amefafanua zaidi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa fedha ili kuwezesha utekelezaji huo kwa Vijiji vyote nchini.
Vilevile amesema kuwa Serikali itapeleka umeme katika maeneo yote yenye shughuli za kijamii na kiuchumi kupitia mradi wa kupeleka umeme kwenye huduma za kijamii, zikiwemo shule, vituo vya afya, misikiti, makanisa na visima vya maji.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Yusuph Ismail ambaye pia ni Meneja Uthibiti na Ufuatiliaji wa Miradi REA amesema Wilaya ya Mbinga imepewa shilingi Bilioni 28.8 kwa ajili ya kupeleka umeme vijiji ambavyo bado havijavikiwa na umeme.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit