WAFANYABIASHARA WA MAZAO MBINGA DC WAPEWA ANGALIZO
Na Silvia Ernest
Wafanyabiashara wa mazao Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wametakiwa kufuata taratibu zilizopo wakati wa kusafirisha mazao ili kuepuka usumbufu pamoja na adhabu ya kulipa faini pindi watakapokiuka taratibu zilizopo.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura alipozungumza na wafanyabiashara hao Ofisi kwake tarehe 4 Julai 2024.
Amesema " kuna baadhi ya wafanyabiashara hawafuati sheria zilizopo wakati wa kusafirisha mazao kuna baadhi hata leseni zimepita muda wake sasa ili tuweze kwenda sawa lazima tufuate taratibu zilizowekwa"
Aidha amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kutoa taarifa pindi wanapogundua wafanyabiashara ambao wanakiuka taratibu hatua ambayo itapelekea kudhibiti upotevu wa mapato.
" Tuendelee kushirikiana haya mapato tunayokusanya ndio tunayotumia kutekeleza miradi yetu ya maendeleo sasa mtu anapofanya biashara kinyume na taratibu tutapata wapi hizo fedha" Amesisitiza
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Divisheni Viwanda na Biashara na Uwekezaji Martina Ngahy amewataka wafanyabiashara hao kulipa ushuru , kuwa na leseni hai pamoja na kibali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga akisisitiza kuwa ofisi yake ipo wazi kuwahudumia muda wote.
Nae Msafiri Turo ambae ni mfanyabishara wa mazao amemshukuru Mkurugenzi Kashushura kwa kukutana na wafanyabiashara hao na kusisitiza kuwa hatua hiyo imesaidia kutatua changamoto kutoka pande zote mbili huku akitoa wito vikao hivyo viwe endelevu.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit