Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Andrew Mbunda amewataka walimu wanaojengewa uwezo wa mtaala mpya wa elimu msingi kushiriki mafunzo hayo kikamilifu pamoja na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wawezeshaji.
Mbunda ametoa rai hiyo tarehe 1 Machi 2024 wakati akizungumza na baadhi ya walimu wanaojengewa uwezo katika moja ya kituo cha mafunzo kilichopo Kata ya Maguu.
Amebainisha kuwa mafunzo haya ni moja ya utekelezaji unaofanywa na Serikali wenye lengo la kurahisisha utekelezaji wa mtaala huo ambao umeanza kutekelezwa rasmi mwezi Januari 2024.
" Kupata mafunzo ni jambo moja na kuyafanyia kazi mafunzo hayo ni jambo jingine tukayatumie mafunzo haya ili kuleta tija katika shule zetu kama ilivyo azma ya Serikali" Amesisitiza
Naye Afisa elimu awali na msingi Mwl.Veronica Justine amebainisha kuwa sambamba na mafunzo hayo tayari Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepokea vitabu vya mtaala mpya wa elimu vitakavyotumika kufundishia wanafunzi wa darasa la awali, la kwanza pamoja na darasa la tatu.
Ameongeza kuwa mtaala huo umezingatia nadharia za ukuaji na ujifunzaji na falsafa ya elimu ya kujitegemea inayosisitiza elimu ya kumuwezesha mtanzania ajitegemee na amudu maisha yake ya kila siku.
Imeandikwa na Silvia Ernest
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
1 Machi, 2024
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit