WANA MUUNGANO WAMSHUKURU RAIS SAMIA UJENZI WA SEKONDARI
Na Silvia Ernest
Wananchi wa vijiji vya Kindambachini, Kizota na Kimara vilivyopo Kata ya Muungano Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ambayo itawaondolea adha wanafunzi kutembea zaidi ya kilomita 10 kwenda katika shule ya Sekondari iliyopo Kata ya jirani.
Wameahidi kutoa ushirikiakiano katika utekelezaji huo ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati ili shule hiyo ifunguliwe mwezi Januari 202.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Paul Kayobo alipozungumza kwa niaba ya wananchi hao tarehe 13 Agosti 2024.
“Tunamshukuru Rais wetu kwa kutuletea hizi fedha kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Kata ya Muungano tulipokea maelekezo kutoka kwa wataalam kutoka Halmashauri na baadhi ya maelekezo tumeshayatekeleza” Amesema Mhe. Kayombo
Wananchi hao tayari wameshashughulikia changamoto ya upatikanaji wa maji ambayo yatatumika katika utekelezaji huo pamoja na kufanya usafi katika eneo ambalo itajengwa shule hiyo na kuahidi kutoa nguvu kazi ili kupunguza gharama za utekelezaji.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Felix Danda amebainisha kuwa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kila Kata inakwa na shule ya Sekondari.
Ameeleza kuwa kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kati ya Kata 29 kata 3 tu hazina shule ya Sekondari ikiwemo Kata ya Muungano ambayo tayari kiasi cha shilingi 560,552,827 kimepokelewa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Sekondari.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit