Na Silvia Ernest
Wananchi wa Kata ya Muungano iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wametoa eneo lenye ukubwa wa ekari 9.5 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ambayo utekelezaji wake upo mbioni kuanza baada ya Halmashauri kupokea Shilingi 1,776,658,827 kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya Kata ya nyoni, Litembo, Muungano na nyumba ya mwalimu Kata ya Kitumbalomo.
Hayo yamebanishwa na Diwani wa Kata ya Muungano Mhe. Paulo Kayombo alipozungumza katika kikao cha kutambulisha mradi wa ujenzi wa shule hiyo kwa wananchi wa Kata hiyo tarehe 17 Julai 2024.
“Sisi wananchi wa Kata hii tumetoa eneo ukubwa wa ekari 9.5 kudhihirisha kuwa tupo tayari kushirikiana na Serikali katika ujenzi huu,sambamba na eneo hili tutashirikiana na Serikali bega kwa bega kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati na katika ubora” Amebainisha Mhe. Kayombo
Naye Diwani wa Kata ya Kitumbalomo Mhe. Denis Kapinga amebainisha kuwa wananchi wa Kata ya Kitumbalomo wameukubali mradi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu ambayo utagharimu 95,000,000 hadi kukamilika kwa kuwa mradi huu utaleta tija katika ujifunzaji na ufundishaji.
Kwa upande wake Yosefa Nsembele mwananchi wa Kata ya Kitumbalomo amepeleka salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kusisitiza kuwa wapo tayari kwa ajili ya utekelezaji.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit