Wananchi kutoka katika Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wamejitokeza kunywa dawa kinga za usubi. zoezi hili limeanza rasmi leo tarehe 17 hadi 23 Agosti 2023.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi hili Mratibu wa magonjwa yasiopewa kipaumbele kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Ngd. Joseph Washa Washa amebainisha kuwa Usubi(ONCHOCERCIASIS) ni ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na minyoo ijulikanayo kwa jina la ONCHOCER VOLVULAS na kuenezwa na inzi wadogo wadogo wanaopatikana katika mazingira machafu katika maeneo ya mito.
Amebainisha dalili za ugojwa wa usubi ni pamoja na kuwashwa mwili, ngozi kuwa na mabakamabaka kama ya kenge pamoja na kubabuka ngozi
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit