Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imewapongeza wananchi wa Kijiji cha Malindindo kilichopo Kata ya Kambarage kwa kuchangia Tshs. 20,000,000 katika ujenzi wa Zahanati ambayo inatarajia kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya 2000 wa Kijiji hicho.
Aidha Kamati hiyo imeiwapongeza wananchi wa Kijiji cha Kibandai A kilichopo Kata ya Maguu kwa kuchangia zaidi ya Mil. 20 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji.
Pongezi hizo zimetolewa 15 Agosti 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambae pia ni diwani wa Kata ya Maguu Mhe. Bahati Mbele wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Amesema “ Hii ndio ari anayoitaka Rais Samia tuendelee kumuunga mkono katika utekelezaji wa miradi mingine iliyopo na itakayokuja kwasababu sisi ndio wanufaika namba moja wa miradi hii”
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji Mtendaji wa Kata ya Kibandai A Rehema Njovu amebainisha kuwa pamoja na fedha hizo Kijiji kilipokea Tshs. 50,000,000 kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ili kukamilisha ujenzi huo ambao wananchi walitekeleza hadi kufikia hatua ya rinta.
Naye Mtendaji wa Kijiji cha Malindindo Cleopatra Lindi amebainisha pamoja na nguvu za wananchi Kijiji kilipokea Tshs. 50,000,000 kutoka Serikali Kuu na Tshs. 7,120,000 kutoka Ofisi ya Mkurugezi Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa ajili ya kumalizia mradi huo.
Akitoa maoni Mjumbe wa Kamati hiyo Diwani wa Kata ya Amani Makoro Mhe. Abrose Nchimbi ameupongeza uongozi wa Kijiji cha Kibandai A kwa kusimamia ujenzi huo akisisitiza kuwa ubora wa Zahanati hiyo unaridhisha na thamani ya fedha imeonekana.
Kwa upande wake Mhe. Michael Komba Diwani wa Kata ya Wukiro na mjumbe wa Kamati ametoa wito kwa uongozi wa Kijiji cha Malindindo na Kibandai A kuweka mkakati na mpango thabiti wa kujenga nyumba za watoa huduma ili watumishi hao wakae karibu na kituo na kuepusha usumbufu wakati wa kutoa huduma.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit