Na Silvia Hyera
Wanawake wa Wilaya ya Mbinga wametakiwa kujikita katika shughuli za kiuchumi ili kuongeza pato la familia lakini pia kuondokana na hali ya utegemezi.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Ally Mangosongo katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Mbinga uliofanyika katika Kata ya Kitura tarehe 13 Septemba 2023.
Amesema" Kwakuwa mwanamke atajikomboa kiuchumi ataondokana na hali ya utegemezi na kuacha kuomba omba fedha kutoka kwa mweza wake bali atashirikiana nae katika kuleta maendeleo ya familia"
Aidha amewataka wanawake hao kutumia fursa za kiuchumi zilizopo Wilaya ya Mbinga katika kubuni biashara zenye tija zitakazoleta ushindani wa kibiashara wenye kuleta maendeleo katika Wilaya ya Mbinga.
Kwa kutambua hilo Mhe. Mangosongo amesema kuwa Wilaya ya Mbinga inaendelea na mkakati wa kuwatafutia masoko wajasiriamali wa Mbinga hasa wanawake.
"Katika Wilaya yetu ya Mbinga tumepanga na tunaendelea kuwatafutia masoko wajasiriamali na hasa wanawake,
Mwaka huu tumeanzisha maonesho ya Nanenane kiwilaya na kupitia maenesho hayo wanawake wengi wajasiriamali walifika na kuuza bidhaa zao" Amesema Magosongo
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit