• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima
  • MIFUMO

ZIARA YA KAMATI YA WATAALAM KATA YA KITURA KUKAGUA MIRADI

Tarehe ya kuwekwa: May 17th, 2021

Kamati ya Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga leo Mei 17, wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya kata ya Kitura, iliyopo Tarafa ya Mbuji ikiwa ni utararatibu wa viongozi hao kutembelea miradi na kusikiliza kero za wananchi Jumatatu ya kila wiki.

Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ya wataalam iliyongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Mwalimu Samwel Komba, ambaye pia ni Afisa Elimu Msingi ni ujenzi wa choo bora cha kisasa (matundu 12) Shule ya Msingi Mzuzu, Zahanati ya Kijiji cha Mahilo, ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja ya walimu Shule ya Msingi Lisau pamoja na jengo la utawala Shule ya Sekondari Kitura, miradi ambayo tayari imeshapelekewa fedha zaidi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya awamu ya kwanza ya utekelezaji wake.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwl. Komba ametoa wito kwa viongozi wa shule, kijiji na kata kuanza mara moja ujenzi wa miradi ambayo tayari fedha zake zimeshatolewa na serikali akitolea mfano ujenzi wa choo cha kisasa shule ya msingi Mzuzu mradi ambao fedha zake kiasi cha shilingi Milioni 13.2 tayari zipo kwenye akaunti ya shule hiyo.

Mwalimu Komba pia amepongeza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa madarasa shule ya msingi Lisau ambapo amesema kwa hatua iliyofikiwa viongozi waliosimamia mradi huo wameitendea haki fedha ya serikali iliyotolewa na kuwataka viongozi hao na viongozi wengine wote kuwajibika kikamilifu kwa kusimamia vilivyo utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao ambapo pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitolea nguvukazi na kuchangia tofali, mchanga, mbao na vifaa vyote nje ya vile vinavyozalishwa viwandani.

Kaimu Mkurugenzi pia amewataka viongozi wa kijiji na kata kuanza mapema mchakato wa kuandaa madawati huku akionya na kutoa angalizo kwa viongozi kuepuka kuchangisha wanafunzi na wazazi wakati shule zinapofunguliwa ambapo Mwenyekiti wa Kijiji wa Kijiji cha Lisau amemhakikishia Kaimu Mkurugenzi kuwa kwa kuanzia tayari maandalizi ya madawati yameshaanza kwa kupitisha maazimio kupitia mkutano mkuu wa kijiji ya kila kitongoji kuchangia madawati mawili ifikapo Julai 30, 2021.

Kwa upande wao wananchi kupitia kwa Diwani wa Kata ya Kitura, Mhe. Alex Ngui wamemshukuru Mkurugenzi na uongozi mzima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kuwapelekea fedha za miradi ya maendeleo na kuomba serikali kuendelea kurahisisha utolewaji wa huduma kwa wananchi kwa kuondoa kero na kupunguza adha ya wananchi mathalani ya kufuata huduma za afya Hospitali ya Litembo kwa wananchi wa Vijiji vya Mahilo na vijiji jirani hasa kipindi cha masika.

Akizungumzia miradi mingi kufikia hatua nzuri ambayo kukamilishwa kwake kuhitaji tu kuwekwa madirisha, dari na kupakwa rangi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amemuagiza Kaimu Mhandisi wa Ujenzi, Bw. Hassan Mateleka kuchukua makisio ya kazi na vifaa vyote vinavyohitaji kukamilisha miradi hiyo na kuwasilisha ofisini kwake ili Halmashauri ione namna bora ya kukamilisha miradi hiyo haraka ikiwezakana ndani ya kipindi cha mwaka huu wa fedha 2020/2021 au mwanzoni mwa mwaka ujao wa fedha wa 2021/2021.

Pia Kamati hiyo imetembelea Chama cha Msingi Lisau (Lisau AMCOS) na kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa chama hicho cha msingi ambacho kimezaliwa kutoka AMCOS Mama ya Mahilo (Mahilo AMCOS) ambapo viongozi hao wamemthibitishia Kaimu Mkurugenzi na timu yake kuwa chama hicho kinaendelea vizuri na utendaji kazi wake na hakuna mgogogoro wowote baina ya wanachama na viongozi wa kijiji na kata hiyo.

Mwenyekiti wa Lisau Amcos Bw. Batwin Hyera amesema Chama hicho tayari kimeanza kupokea kahawa tangu Mei 5 kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa kahawa huku akisema kwa msimu uliopita chama kiliweza kulipa wanachama wake wote kwa bei ya juu ya shilingi 5,200/= kwa kilo na kwamba Amcos hiyo pia imekua ikichangia ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa Shule ya Msingi Lisau na Sekondari ya Kitura ikiwemo kuchangia vifaa vya ujenzi na fedha taslimu

Imeandikwa na

Salum Said

Afisa Habari, Mbinga D.C

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI September 17, 2024
  • TANGAZO LA HESABU MBINGA DC July 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA MKATABA NAFASI YA MKUSANYA USHURU January 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA- DEREVA NAFASI 2 January 25, 2024
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI KASHUSHURA ATOA MSISITIZO MATUMIZI YA NISHATI SAFI SHULENI

    February 15, 2025
  • MAAFISA TUME WATEMBELEA MBINGA DC

    January 08, 2025
  • WAANDISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA ANGALIZO

    January 09, 2025
  • KASHUSHURA AWAPONGEZA WANANCHI UJENZI WA SHULE

    September 10, 2024
  • Tazama zote/kote

Video

UGAWAJI WA MKAA MBADALA
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit