Na Silvia Ernest
Watendaji wa Kata na Vijiji wametakiwa kuhakikisha taarifa za mapato na matumizi zinatolewa kwa wananchi kupitia vikao vya kisheria ili kuleta uwazi na uelewa wa pamoja wa matumizi ya fedha katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Agizo hilo limetolewa tarehe 14 Mei 2024 na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Rwiza alipozungumza na wananchi wa Kijiji cha Luhagara Kata ya Litumbandyosi.
" Kila mtendaji katika halmshauri hii anatakiwa kusoma taarifa ya mapato na matumizi, wananchi wana haki ya kujua namna fedha zinavyotumika katika maeneo yao" Amebainisha
Pia ametumia nafasi hiyo kuwataka Wakuu wa shule na Walimu wakuu kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi na kuhakikisha idadi ya wanafunzi wanaoanza elimu ya msingi au sekondari inalingana na idadi ya wanafunzi watakaohitimu.
Akizungumza na wananchi hao Mkurugenzi Rwiza ameahidi kumalizia ukamilishaji wa darasa moja lililopo shule ya Msingi Luhagara ili dasara hilo litumike kama lilivyo kusudio la wananchi hao.
Sambamba na hilo ameahidi kuwasiliana na Shirika la Umeme Wilaya ya Mbinga katika kutatua changamoto ya ukosefu wa umeme Shule ya Sekondari Luhagara hatua ambayo itaimarisha ujifunzaji na ufundishaji.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit