Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga siku ya Jumatano tarehe 9 Novemba 2022, Baraza la Madiwani liliketi katika kikao chake cha kawaida cha robo ya kwanza kujadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2022/2023.
Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ulioko Kiamili na kuongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mhe. Desderius Haule na Katibu wa Baraza hilo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Juma Haji Juma, Kikao hicho kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Pamoja na mambo mbali mbali yaliyojadiliwa na Baraza hilo, Pia limeishauri Serikali kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA kuchunguza na kumchukulia hatua kandarasi Kisomi Engeneering Ltd kutokana na utekelezaji ulio chini ya kiwango wa miradi ya barabara na madaraja kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga. Aidha, Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Mbinga Mhandisi Isack Mwita amesema tayari hatua kadhaa zimeanza kuchukuliwa ikiwemo shauri hilo kufikishwa Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Mbinga, sambamba na kuipatia kampuni nyingine za kandarasi ambazo awali alipatiwa mkandarasi Kisomi Engineering Ltd.
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga liligeuka kuwa Kamati ili kujadili shauri la utoro la mtumishi Reginald Sabas Komba ambapo kupitia taarifa ya maamuzi ya kamati, Mwenyekiti Mhe. Desderius Haule aliutangazia imma kuwa wamejiridhisha juu ya mashitaka hayo hivyo wameamua kumfuta kazi mtumishi huyo aliyekua Mtendaji wa Kijiji cha Kimara Kata ya Muungano kwa kosa la kutokuwepo kazini muda mrefu.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit