Kamati ya fedha , mipango na uchumi imefanya ziara ya siku 2 (30/May/2019 - 31/May/2019)kukagua miradi inayotekelezwa ndani ya Halmashauri. Halmashauri inatekeleza miradi mingi ikiwepo inayotekelezwa
na serikali na ile inayotekelezwa na Halmashauri. Halmashauri imepokea fedha kiasi cha milioni 400 za kujenga kituo cha afya mapera, zaidi ya milioni 160 za ujenzi wa bwalo na maktaba sekondari ya Ruanda na
fedha za kukamilisha maboma na P4R. Wakikagua miradi hiyo ikiwepo kituo cha afya Mapera , Sekondari ya Langiro,sekondari Mkoha , sekondari ya Luli, sekondari ya Kiamili, Ujenzi wa choo shule ya msingi kitai,
Ujenzi wa choo bandari kavu.Ujenzi wa madarasa sekondari ya ndongosi na Ujenzi sekondari ya Ruanda( Maktaba na Bwalo).
Aidha mwenyekiti wa Halmashauri aliwataka wananchi kushirikiana na serikali ili kukamilisha miradi hasa inapohitajika wao kujitole "ndungu zangu wa Ndongosi, maendeleo yataletwa na nyinyi wenyewe,msisubiri mtu aje kuwaletea maendeleo" alisema mwenyekiti baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa madarasa ambao unasuasua . Wananchi wa Ndongosi wameahidi kuongeza kasi ikiwepo mtendaji kata kuamia katika kijiji cha Ndongosi ili kusimamia kwa karibu shughuli za ujenzi. Baadhi ya picha za miradi iliyotembelewa zimeambatanisha hapa chin
Kamati ikakagua mradi wa Maktaba Ruanda sekondari fundi atakiwa kuongeza kasi ya ujenzi wa maktaba hiyo ili jengo likamilike kwa wakati
Mkuu wa gereza Kitai SSP Shayo akitoa maelezo namna wanavyoshiriki ujenzi wa choo katika sm Kitai, ujenzi huu ulitokana na wanafanzi wa sm Kitai kutoa malalamiko mbele ya Rais wa Jamhuri y muungano wa Tanzania
Mhe. Pombe Joseph Magufuli nae kutoa milioni 5
Mganga Mkuu wa kituo cha afya Mapera Doc. Charles Sanga(mwenye koti jeupe) akitoa maelezo kuhusu kituo cha Mapera kwa mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ambrose Mtalazaki
Ujenzi wa bwalo: kamati ya mipango na fedha ikiongozana na timu ya wataalam wakikagua mradi wa Bwalo katika sekondari ya Ruanda
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit