Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Christina Mndeme amefanya ziara ya kikazi ya siku 2 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga leo tarehe 5/Nov/2018. Ziara hii ya Mkuu wa Mkuu wa mkoa inahusisha kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero mbali mbali za wananchi.
Aidha Mh. Mkuu wa Mkoa Bi. Christina Mndeme amesisitiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuunga jitihada za serikali ya awamu ya tano inayohakikisha ilani ya chama inatekelezwa kwa kuotoa fedha na kutekeleza miradi mbali mbali " serikali inatoa fedha za elimu bure, kwa mara ya kwanza umeme wa gridi ya Taifa unawaka ndani ya Ruvuma, huduma za afya zinaboreshwa kwani zaidi ya bilioni 5 zimetolewa kuimarisha miradi y afya"alisema Mh. Mkuu wa Mkoa.
Pia aliwaasa wananchi wanao fanya mambo ambayo yanalengo la kurudisha maendeleo nyuma, kasema tayari kuna watu 10 wanaofanya biashara ya magoma wamekamatwa na wamepelekwa mahakamani. '' Wale wote watakaouza kahawa kwa kwa mfumo haramu, tutawakamata kwa mtindo wa kata funua, yaani atapigwa gwara kisha ataruka juu atafikia pua kisha atawekwa rokapu na kupelekwa mahakamani" alisisitiza mkuu wa Mkoa.
Aidha amewahakikishia wakulima wa mazao ya mbali mbali kuwa pembejeo za kilimo zitakuwepo za kutosha kwakuwa tayari wazabuni wameshapatikana na tayari wameanza kusambaza pembejeo za kilimo.
Endelea kupitia tovuti hii uone taarifa zaidi
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit